Kumb. Na EA.7/96/01/H/18 13 Novemba, 2014
7.0 KATIBU WA KAMATI DARAJA LA II (COMMITTEE CLERK GRADE II) – NAFASI 2
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kuandaa ratiba ya vikao vyote vya Halmashauri na kamati zote kwa kushauriana na Mkurugenzi Mtendaji
• Kuandika Mihutasari ya vikao vya Halmashauri
• Kuweka Kumbukumbu za vikao vya Halmashauri nma kamati zake.
• Kutunza Vifaa vyote vinavyohusiana na mikutano.
• Kuhifadhi orordha ya mahudhurio ya Madiwani na Wataalamu.
• Kutoa ratiba ya ufuatiliaji na utekelezaji wa maazimio
• Kutunza Kanuni za Mikutano.
• Kusimamia "cutting" za mihutasari.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada /Stashahada ya Juu ya Sheria au Utawala kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 27 Novemba, 2014
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu, | AU | Secretary, |
Sekretariati ya Ajira katika | | Public Service Recruitment |
Utumishi wa Umma, | | Secretariat, |
SLP.63100, | | P.O.Box 63100 |
Dar es Salaam. | | Dar es Salaam. |
0 comments:
Post a Comment