WATUMISHI 228 wa Idara ya Uhamiaji wa ngazi ya Konstebo na Koplo, walioshinda usaili na kuitwa kazini, wamefukuzwa kazi. Hatua hiyo imetangazwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil, baada ya kubainika kuwa baadhi ya watumishi hao, waliajiriwa kwa upendeleo kwa kuwa walikuwa ndugu, jamaa na watoto wa waliowasaili.
Tangazo hilo limekuja siku moja, baada ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kuweka bayana mapendekezo ya Sheria ya Mgongano wa Maslahi, ambayo ikipita bila vikwazo, itazuia uchakachuaji huo.
Mapendekezo ya sheria hiyo, pamoja na mambo mengine, yanakusudia kuzuia viongozi au watumishi wa umma wenye dhamana ya ajira, kushiriki katika mchakato wa ajira unaohusisha familia, rafiki au ndugu.
Abdulwakil alisema, kati ya ajira hizo 228 zilizofutwa, ajira 28 ni zilizotangazwa na kujazwa kwa upande wa Ofisi ya Uhamiaji Zanzibar. " Tume imebaini kuwa baadhi ya wasailiwa waliopata alama za juu za ufaulu, hawakuitwa kazini na hakukuwa na sababu maalumu zilizotolewa," alisema.
Alisema kamati hiyo pia imebaini kuwa baadhi ya waombaji wenye umri mkubwa zaidi ya uliotajwa kwenye matangazo, miaka 25 kwa kostebo na miaka 30 kwa koplo, walisailiwa na kuitwa kazini.
Awali tuhuma hizo zilisambaa katika mitandao, zikitaja majina kabisa ya walioajiriwa na undugu zao na waliowaajiri na kuibua hisia za upendeleo katika ofisi hizo za umma.
Baada ya hapo Julai 28, mwaka huu Abdulwakil alitoa taarifa ya kusitisha ajira hizo, na kuunda kamati ndogo ya uchunguzi, kubaini ukweli wa taarifa hizo za mtandaoni.
"Waombaji wote walioitwa na kutakiwa kuripoti katika ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Agosti 6, 2014, wanatakiwa kusubiri hadi hapo watakapotangaziwa tena baada ya uchunguzi kukamilika na uamuzi kufanyika," alisema Abdulwakil katika taarifa yake aliyoitoa kusitisha ajira hizo.
Baada ya kusitishwa kwa ajira hizo, wakati uchunguzi ukifanyika, gazeti hili lilipokea taarifa kwamba matukio hayo yapo na yanaendelea katika ofisi, taasisi na mashirika ya umma.
Juzi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imekiri kuwa hakuna Sheria inayoweka masharti ya kumzuia kiongozi au mtumishi wa umma, mwenye dhamana katika ajira kushiriki katika mchakato wa ajira ya watu alio na uhusiano nao.
Kutokana na udhaifu huo, Sekretarieti hiyo imeeleza kuwa kumekuwa na changamoto kadhaa, ikiwemo upendeleo, rushwa na mgongano wa maslahi, Changamoto nyingine ni kupotea haki za ajira kwa waombaji wenye sifa na kupata watumishi wa umma wasio na sifa.
Kutokana na changamoto hiyo, Sekretarieti hiyo iliyo chini ya Ofisi ya Rais, imependekeza Sheria mpya ya Mgongano wa Maslahi, izuie viongozi au watumishi wa umma wenye dhamana ya ajira, kushiriki katika mchakato wa ajira unaohusisha familia, rafiki au ndugu.
"Inapendekezwa Sheria ieleze kuwa panapotokea mazingira yanayohitaji uamuzi kuhusu ajira ya wanafamilia au ndugu wa kiongozi au mtumishi wa umma katika taasisi yoyote ya umma, kiongozi au mtumishi husika, atamke uhusiano uliopo baina yake na msailiwa na kujiondoa katika mchakato wa ajira husika," imeelezwa klatika mapendekezo ya Sekretarieti hiyo.
Baada ya kubaini ukiukwaji huo wa maadili, Abdulwakil alisema ajira hizo zitatangazwa upya na mchakato wa ajira hizo utaendeshwa na wizara.
Alipoulizwa hatua gani zitachukuliwa kwa watendaji waliotumia nafasi zao vibaya, alisema watu hao watatakiwa kujieleza kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.
Alipoulizwa kama ni kosa kwa mtoto wa mtumishi kuomba kazi hizo, Abdulwakil alisema hilo si kosa na kuwataka waliobainika kuwa ni ndugu wa maofisa kuomba upya.
"Si kosa kwa mtoto au ndugu wa ofisa kuomba kazi, tatizo lilijitokeza ni kuwa watu waliowasahili ndio hao hao waliowapitisha, siwezi kumpa mtihani mwanangu na kumsahihishia mwenyewe.
"Awamu hii itasimamiwa na Wizara ambayo itakuwa msimamizi huru, sasa wale waliobainika kuwa ndungu za maofisa wanaweza kuomba ili kushinda," alisema.
CHANZO: Habari leo

0 comments:
Post a Comment