Tuesday, September 10, 2013

Vita ya mauzo ya Jezi Ozil vs Bale .


Vita ya mauzo ya Jezi Ozil vs Bale .
bale jezi
Ikiwa imepita wiki moja tangu klabu za Real Madrid na Arsenal zilipokamilisha usajili wa wachezaji waliobadilishana ligi za England na Hispania Gareth Bale na Mesut Ozil kwenye siku ya mwisho ya dirisha kubw ala usajili , tayari malipo ya fedha zilizotumika kusajili wachezaji hao yameanza kuonekana .

Kwa mujibu wa maduka mawili makubwa ya jezi za wachezaji wa timu mbalimbali zinazonunuliwa na mashabiki  kwenye mtandao ya UKSoccershop.com na Worldsoccershop jezi ya Arsenal yenye jina la mchezaji Mesut Ozil imeonekana kufanya vizuri sokoni kuliko ya Gareth Bale ambayo ilianza kuuzwa wiki mbili kabla ya kutambulishwa kwa mchezaji huyo .
Tayari jezi ya Mesut Ozil imeeingizia Arsenal zaidi ya paundi milioni baada ya mashabiki wa timu hiyo kuichangamkia huku jezi ya Gareth Bale kwa Real Madrid ikionekana kudoda ambapo inanunuliwa kwa kasi ya chini.
Hali hii inachangiwa na ukweli kuwa Mesut Ozil ametokea kuwa kivutio kwa mashabiki wa Arsenal waliofurahishwa sana na kitendo cha Kocha Arsene Wenger kutumia paundi milioni 42 kumsajili mchezaji mwenye hadi ya "KisuperStar" tofauti na Real Madrid ambao wamemsajili mchezaji toka Wales ambaye pamoja na kipanji , uwezo na kiwango chake cha juu bado hana jina kubwa na mvuto wa umaarufu walio nao wachezaji wengine .
Jezi ya Arsenal ya Mchezaji              Mesut Ozil inaonekana kufanya vizuri sokoni kuliko ya Gareth              Bale.

Jezi ya Arsenal ya Mchezaji Mesut Ozil inaonekana kufanya vizuri sokoni kuliko ya Gareth Bale.
Manunuzi ya jezi za wachezaji ni kipimo tosha cha jinsi ambavyo mchezaji anakubalika miongoni mwa mashabiki wa timu alikosajiliwa na mara nyingi pia yamechangia kurejesha fedha zilizotumika kumnunua mchezaji .
 Mfano Mzuri wa Hili ni kiungo mshambuliaji wa Brazil Neymar ambaye hadi sasa mauzo ya jezi yake ya Barcelona tayari yamesharudisha hela iliyotumika kumsajili kwa karibu mara mbili.
Usajili wa Gareth Bale toka klabu ya Tottenham Hotspurs kwenda klabu ya Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 86 umepokewa kwa hisia tofauti ambapo baadhi ya watu maarufu kwenye mchezo wa soka wameonyesha kutokukubaliana na kitendo cha Madrid kumwaga fedha kiasi hicho kwa Bale . Mmoja wa watu waliohoji bei ya Bale ni kocha msaidizi wa Madrid na Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo ambaye amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa Zinedine Zidane ambaye alinukuliwa akisema kuwa haamini kama kweli Bale anaweza kuwa na thamani kama hiyo kwani hata yeye mwenyewe (zidane ) wakati aliokuwa anacheza hakuwa na thamani ya bei ya Bale pamoja na uwezo wake mkubwa.
Orodha ya Wachezaji walioongoza kwa mauzo ya Jezi nchini England msimu Uliopita.
1.Robin Van Persie.(Man United)
2.Wayne Rooney .(Man United)
3.Shinji Kagawa.(Man United)
4.Sergio Aguerro.(Man City)
5.Fernando Torres (Chelsea)
6.Edin Hazzard. (Chelsea)
8.Jack Wilshere(Arsenal)
9.Alex Oxlade Chamberlain(Arsenal)
10.Santiago Cazorla.(Arsenal)



0 comments:

Post a Comment