Monday, August 26, 2013

CHAZ BABA AAGA UKAPERA, TAZAMA PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA SIKU YA HARUSI HAPA


CHAZ BABA AAGA UKAPERA, TAZAMA PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA SIKU YA HARUSI HAPA

101-2Chaz na mkewe kwenye misa.
181-2Wakionyesha vyeti vyao vya ndoa.
171-2Baada ya misa wakiwa na furaha kuu.
RAIS wa bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel Cyprian 'Chaz Baba', juzikati aliua ndege wawili kwa wakati mmoja pale alipotoa burudani ya nguvu katika sherehe ya harusi yake iliyofanyika katika ukumbi wa Mirado Hall uliopo Sinza Makaburini jijini Dar, na pia kutinga katika ukumbi wa Mango Gadern Kinondoni jijini Dar ambapo Twanga Pepeta walikuwa wakiendeleza wimbi la burudani katika ukumbi huo.
Tukio hilo la Chaz kutinga katika ukumbi wa Mango liliwashangaza wengi kwani kwa wakati ule Chaz alitakiwa kwenda kupumzika kutokana na mkewe kuonekana amechoka kwa sababu ya ujauzito wake.
"Shemeji yetu anaonekana kachoka sana lakini Chaz ndio kwanza anaonekana hana hata muda wa kwenda kulala mapema" alisema shabiki mmoja aliyekuwa ndani ya ukumbi.
Chaz Baba alifunga ndoa na Rehema Sospeter Marwa, siku ya Agosti 24, mwaka huu katika kanisa la St Peters jijini Dar es Salaam.



Related Posts:

0 comments:

Post a Comment