Wednesday, October 3, 2012

ALIYEKUWA MTUMISHI WA BABA MTAKATIFU AKANA MASHITAKA YANAYOMKABILI.




 Mtumishi wa baba mtakatifu Benedict wa 16 anayetuhumiwa kwa wizi wa nyaraka za siri za kanisa Katoliki amesema hana hatia ya kosa hilo.
Akitoa ushahidi mbele ya mahakama mjini Vatican, mtumishi huyo Paolo Gabriel (mwenye suti ya kijivu pichani) amesema kuwa hana  mahusiano ya moja kwa moja na wizi huo.
Mtumishi huyo kwa sasa anashitakiwa kwa kosa la kuiba na kuvujisha nyaraka wakati wa utumishi wake katika ofisi ya baba mtakatifu Benedict 16.
Ikiwa ni siku ya pili ya mashitaka yake mahakamani, Gabriel ameiambia mahakama kuwa ana hatia ya kuisaliti imani ya baba mtakatifu kwake, lakini kamwe hana hatia ya wizi wa kuchochewa. 

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment