WATU watatu wakiwemo WANAFUNZI wawili wa shule ya msingi wilayani Kasulu na mkulima mmoja katika wilaya hiyo wamefariki dunia kufuatia kupigwa na radi ambapo mtu mmoja amejeruhiwa katika hilo.
Akizungumza mjini hapa na Waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Fraiser Kashai aliwataja watu hao waliofariki kuwa ni Jackline Leonald mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Rusesa wilaya ya kasulu na ndugu yake Maria Leonald ambao walikutwa na mauti hayo wakiwa njiani kurejea nyumbani wakitokea shambani.
Sambamba na hao Kamanda huyo wa polisi alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefariki katika tukio hilo kuwa ni Zuwena Cosmas Mwanafunzi wa shule ya msingi Kagera Nkanda wilayani Kasulu ambapo pia radi hiyo ilmjeruhi Rahel Lucas (10) mkazi wa kijiji hicho cha Kagera Nkanda ambaye anapatiwa matibabu kwenye zahanati hiyo ya kijijk.
Kamanda Kashai alisema kuwa matukio hayo yaliyotokea majira ya kati ya saa nne asubuhi na saa mchana yanafuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika maeneo hayo ambayo iliambata na radi kubwa iliyokuwa ikipiga.
mwisho.

0 comments:
Post a Comment