Jeneza lenye mwili wa marehemu Willy Edward likiingizwa ndani baada ya kuwasili nyumbani kwao Mugumu, wilayani Serengeti Mkoani Mara.Marehemu Willy anataraji kuzikwa leo majira ya Saa 9 alasiri,kwenye eneo la kiwanja cha Nyumba yao,eneo la Molotonga.
Mdogo wa marehemu Willy Edward (kushoto) akilia huku akilakiwa na ndugu yake baada ya mwili wa marehemu Willy Edward kuwasili nyumbani kwao
Baadhi ya ndugu wa marehemu Willy Edward wakiangua vilio baada mwili kuwasili nyumbani kwao Mugumu, Serengeti
Mzee Edward Ogunde, baba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akifarijiwa na mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapicha gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania, Anicetus Mwesa nyumbani kwao marehemu, Mugumu Mjini, wilayani Serengeti jana. Willy anazikwa leo eneo la nyumba yao karibu na kaburi la mamake. Katikati ni mdogo wa marehemu, Essey Ogunde.
Mmoja wa wazee wa Kijaluo,alietambulika kwa jina moja la Noah akitumbuiza kwenye msiba kwa kutumia kipaza sauti alichokitengeneza. Vijana wakichimba kaburi utakamohifadhiwa mwili wa mpendwa wetu Willy Edward katika viwanja vya nyumba yao eneo la Motolonga, mjini Mugumu. Marehemu Willy Edward aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo atazikwa leo saa 9 alasiri. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.
Picha na Richard Mwaikenda.
Picha na Richard Mwaikenda.
0 comments:
Post a Comment