Sunday, May 13, 2012

Mapigano yachacha nchini Congo


Hali katika sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inasemekana ni tete kutokana na taarifa kuwa mapigano kati ya wanajeshi waasi wanaomuunga mkono mwanajeshi mtoro Jenerali Bosco Ntaganda na majeshi ya serikali yanaendelea.

Bosco Ntaganda

Mapigano hayo yamepamba moto wakati muda uliowekwa wa wapiganaji wa Ntaganda kujisalimisha kumalizika jana Alhamisi.

Taarifa kutoka mpaka wa Uganda na Jamhuri ya kidemokasi ya Congo wa Nabunanana, zinaeleza kuwa mapigano makali yanaendelea ndani mwa Kongo .

Hali hiyo imesababisha raia wengi wa Congo kukimbilia usalama wao nchini Uganda.



0 comments:

Post a Comment