Friday, April 27, 2012

UPDATES HUKUMU YA TUNDU LISSU.


Jaji amemaliza: LISSU AMESHINDA, MUNGU AWABARIKI MLIONIOMBEA NIWAFIKISHIE HAYA

HOJA YA TISA, Kama Mgombea wa walalamikaji (CCM) alikataa kusaini matokeo. Hoja hii haipaswi kunipotezea mud asana. Njau hakuhudhuria, aliwakilishwa na mlalamikaji wa kwanza ambaye alikataa kusaini matokeo. Wakili wa serikali alisema, kukataa pekee kusaini matokeo hakusaidii kutengua matokeo. Hivyo hata hoja ya tisa naitupilia mbali. Haikuwa sahihi.

Hoja ilitolewa hapa, kuwa mawakala walikula kiapo kwa hakimu. Walalamikaji walisema kuwa walipaswa kula kiapo kwa msimamizi wa uchaguzi. Je kuapishwa na hakimu kunabatilisha matokeo? Hoja zilizotolewa na mawakili wa serikali walisema Hakimu ana mamlaka ya kutoa viapo. Binafsi nasema kuwa waliotunga sheria hawakumaanisha kuwa Mahakimu hawaruhusiwi kuapisha mawakala, vinginevyo kungekuwepo fomu ya hakimu tu. Lakini fomu zinaonyesha hakimu, Msimamizi wa uchaguzi na Msimamizi msaidizi, fomu inatambulika kisheria, kwa sheria ya Uchaguzi. Hii haihusiani na zoezi la uchaguzi. Katika kesi ya Prince bagenda Vs Wilson masilingi, katika kesi hii mawakala walifanya kazi bila kuapishwa, na ilichukuliwa kuwa sehemu ya kutengua uchaguzi, angalia pg 240. Kwa lugha yake jaji alisema hawakuwa na mamlaka halali, lawful mandate, lakini ilisaidia kutengua, na mwanasheria wa serikali alihusika katika hili. Maelezo hayo yanatofautiana na kesi iliyo mbele yangu, jimbo la Singida mashariki mawakala walikula kiapo, na walikuwa na mamlaka halali. Hivyo hoja hii naitupilia mbali

Hoja ya 10, Hoja zote hazikutbithitishwa, HIVYO, UCHAGUZI ULIKUWA WA HAKI, NA TUNDU LISSU NI MBUNGE HALALI NA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA WA HAKI, HIVYO SIWEZI KUTENGUA.
Hoja ZOTE zimetupiliwa mbali.

0 comments:

Post a Comment