Wednesday, October 5, 2011

] Mashangingi ya Serikali

Aibu yetu, aibu yao?

  Hii ni aibu,

Na ninamaswali kadaa.

La kwanza: Hizo namba 484 ARX ni za gari gani? Zimepatikanaje na wapi? Kwa utaratibu upi? Ikiwa hazikutolewa na TRA inamaana kuna mtu ameghushi? Inawezekanaje gari likwa na kadi mbili? Au gari za serikali hazinaga kadi? Ikiwa zimeghushiwa[forged] nani awajibike? TRA, Ofisa wa Serikali aliyekabidhiwa gari STK 4431 au dereva wake? Kama hali ni hii tuna uhakika gani kuwa namba za magari yetu binafsi nazo hazitumiwi kuficha ufisadi? Ikitokea ajali au gari kama hili likitumika kwenye uhalifu – mwenye gari lililosajiliwa kihalali kama T484 ARX ataepukaje kubambikiwa kesi kuwa gari lake lilihusika katika uhalifu?; je kitendo cha serikali kubandika namba feki katika magari yake kinamnufaisha nani? Na je siyo uhuni? Kitendo hiki kinamfundisha nini mwananchi wa kawaida? Ikiwa serikali inaendeshwa kihuni jamii yetu itaponaje?

Kwa sasa niishie hapa

Lahaula! Aibu gani hii? Alikua ameficha, ikafichuka!


0 comments:

Post a Comment