Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa daraja la mto Sibiti ambalo linaunganisha mikoa ya Shinyanga, Mara, Mayara , Arusha na Singida yenyewe katika wilaya ya Mkalama ambalo linajengwa na mkandarasi kutoka nchi za Asia kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 16 za kitanzania, Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Tabora, Singida na Manyara akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo, kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 na kuimarisha chama akiongozana na Katbu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida Mh. Parseko Kone(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MKALAMA-SINGIDA)Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea kupata maelezo kutoka kwa viongozi wa mkoa wa Singida kuhusu ujenzi wa Daraja la mto Sibiti wilayani Mkalama
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia akimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Singida Mh. Parseko Kone wakati alipokagua ujenzi wa daraja la mto Sibiti wilayani Mkalama, wapili kulia ni Mwigulu Nchemba Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki na anayefuatia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Gumanga.Mwigulu Nchemba mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi na Naibu Katibu mkuu wa CCM akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Gumanga.Katikati Mwigulu Nchemba mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi na Naibu Katibu mkuu wa CCM, kulia mjumbe wa kamati kuu CCM Khadija Abood kulia na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata wakipata kifungua kinywa kwa mwenyekiti wa shina namba tano Fatma Khamis.Baadhi ya waandishi wa habari na wananchi wakiwa kandokando ya mto Sibiti wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa daraja hilo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na mwenyekiti wa shina namba tano Fatma Khamis wakipata kifungua kinywa wakati katibu mkuu huyo alipomtembelea mwenyekiti huyo katika shina lake, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida Mh. Parseko Kone na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Ndugu Mgana Msindai.Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Gumanga.Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.Wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano huo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma orodha ya vijiji vitakavyopata umeme katika wilaya ya Mkalama mkoani Singida.Baadhi ya waluiokuwa wanachama wa chama cha CHADEMA wakijieleza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati waliporejesha kadi zao za CHADEMA na kujiunga na CCM , kulia ni Mwigulu Nchemba mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki.Kwaya kutoka kata ya Nduguti wakiimba wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyoWananchi wakifuatilia matukio ya mkutano huo.Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwaeleza jambo wananchi huku akiwa naMwigulu Nchemba mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi na Naibu Katibu mkuu wa CCMWananchi wakiwa katika mkutano huo katika kata ya NdugutiKatibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi mbele na Mwigulu Nchemba mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki katikati akikagua ujenzi wa jengo la hoteli la mjasiriamali Bw. Charles Mtaturu linalojengwa katika kata ya Nduguti.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifunua pazia kwa pamoja na Bw. Charles Mtaturu mmiliki wa jengo la hoteli linalojengwa katika kata ya NduutiWananchi wakinyoosha mikono yao juu kuashiiria kufurahia hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Nkungi wilayani Mkalama.Wananchi wakifuatilia hotuba za viongozi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi katika kata ya Nkungi. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika kata ya Nkungi wilayani Mkalama mkoani Singida leo.
0 comments:
Post a Comment