Wednesday, October 10, 2012

Anwani za Makazi Duniani Kuboresha Maisha ya Watu Duniani


Balozi Maalumu wa Umoja wa Posta Duniani, Mh. Prof. Anna Tibaijuka akiwasilisha Tamko la Umoja wa Posta Duniani la Kutoa Anwani za Makazi KWA watu wote duniani.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano Mkuu wa 25 wa Umoja wa Posta Duniani ukimsikiliza Mh.Prof. Anna Tibaijuka akiwasilisha Tamko la UPU kuhusu anwani za Makazi. Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof. Makame Mbarawa,wa pili kulia. Wengine ni Prof. John Nkoma, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, wa kwanza kushoto, Prof. Patrick Makungu, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, (wa tatu toka kutoka kulia, anayefuata ni Bwana Deos Mndeme, Postamasta Mkuu Tanzania, anayefuata ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPC Dr. Yamungu Kayandabila, anayefuata Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dr. Vuai Lila na mwisho ni Mkurugenzi wa Huduma za Posta TCRA.
Wawakilishi wa nchi mbalimbali duniani wakimsikikiliza Balozi Maalum wa Umoja wa Nchi wanachama wa UMoja wa Posta Duniani akiwasilisha Tamko la Umoja wa Posta Duniani la Kutoa Anwani A Makazi KWA watu wote duniani.

Na Innocent Mungy - Doha, Qatar 

Balozi Maalumu wa Umoja wa Posta Duniani, Mh. Prof. Anna Tibaijuka, ameyahimiza Mataifa yote duniani kuhakikisha wanaboresha maisha ya watu wake kwa kuweka anwani za makazi na posti kodi zenye kukidhi mahitaji mbalimbali ya maendeleo ya raia wake. 

 Akiwasilisha Tamko la Doha La Umoja wa Posta Duniani la Kutoa anwani kwa watu wote, Mh. Tibaijuka ambae pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, amezishauri nchi wanachama wa UPU kuhakikisha kila raia anatambuliwa alipo na kuhakikishiwa usalama wake na kujumuishwa kwenye mipango ya maendeleo ya nchi yake. 

Amesema, watu kukosa anwani za makazi kunawakwamisha katika shughuli za maendelo kama vile uwezo wa kutambuliwa ili kupata huduma za msingi za maisha yao kama vile shule, maji na huduma mbalimbali za jamii. Amezitaja huduma zingine kuwa ni pamoja na utambulisho wa makazi rasmi ili kuweza kupata mikopo kutoka katika mabenki yanayoshindwa kutoa mikopo kutokana na wengi wa raia kukosa utambulisho wa wanakokaa. 

Aidha amesema, kutokana na watu wengi zaidi kuhamia mijini kutoka vijijini, Serikali hazina budi kujipanga kupitia program za mipango miji ili kudhibiti makazi holela ambayo hayawezi kutambuliwa rasmi kutokana na kutokuwa na miundo mbinu yeye ubora KWA maisha ya watu. 

Prof. Tibaijuka pia amezihimiza nchi wanachama wa UPU kuwekeza katika kuwa na mfumo thabiti wa anwani za makazi na posti kodi ili mfumo huo uwezo kuboresha maisha ya watu hata kwa huduma za afya za dharura, usalama na urahisi wa kutoa huduma za uokoaji wa watu wakati wa dharura.

 Mh. Prof. Tibaijuka amesema Tanzania tayari imeanza kutekeleza programu wa anwani za makazi na imedhamiria programu hii kukamilika kwa mafanikio makubwa. Tayari miji ya Arusha na Dodoma imeanza utekelezaji wa majaribio na hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizindua utekelezaji wa utoaji wa anwani za makazi KWA mkoa wa Dar es salaam ambapomaliwaagiza watendaji wa jiji la Dar es salaam kuanzia kutoa majina KWA MTAA yore jijini. 

Nchi mbalimbali zimezungumza kufungua mkono Tamko hilo, ikiwemo Costarica iliyopendekeza kuwashurikisha wananchi, wafanyibiashara na taasisi mbalimbali ili kufanikisha mpango wa anwani za makazi kwa kila mwananchi duniani.

 Leo jioni, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof. Makame Mbarawa anatarajia kuhutubia mkutano huu kutoa taarifa ya maendeleo ya huduma za Posta Tanzania na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ndogo ya Posta duniani, hasa nchi kama Tanzania.

0 comments:

Post a Comment