Na Father Kidevu Blog, Monduli
Mrembo wa Mkoa wa Manyara, na mwakilishi wa Kanda ya Kaskazini, Lucy Stephano usiku wa kuamkia leo amenyakua taji la Redds Miss Photogenic 2012 na kuwa mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali ya shindano la Redds Miss Tanzania 2012.
Lucy amefanikiwa kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2012.
Shindano hilo dogo la Haiba ya Picha “Miss Photogenic” alipatikana baada ya jopo la majaji ambao ni wapiga picha mashuhuri nchini Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki.
Mapema akitaja majina ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha Othman Michuzi na Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.
Dalili za kuonesha kuwa Lucy amekubalika hata kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka wakati Mroki akitaja majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na lilipotajwa jina lake ukumbi wa Emanyata uliofurika wakazi wa mji wa Monduli na warembo ulilipuka kwa kwashangwe.
Warembo watano walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Magdalena Roy, Lightness Michael, Babylove Kalala, Diana Hussein na Lucy Stephano.
Warembo wa Redds Miss Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top Model linalotaraji kufanyika Oktoba 13 2012, katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.
Mataji mengine yatakayo waniwa na warembo hao na washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu fainali ni Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.
Taji la Miss Photogenic lilikuwa linashikiliwa na mrembo Stacy Mabula kutoka Shinyanga na Kanda ya Ziwa.
Fainali za mwaka huu za Redds Miss Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Blue Peal Ubungo jijini Dar es Salaam Novemba 2, 2012.
0 comments:
Post a Comment