Monday, March 9, 2015

AFISA MTENDAJI WA KIJIJI



AFISA MTENDAJI WA KIJIJI
Halmashauri Ya Wilaya Ya Lindi

(Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya)


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, anawatangazia watanzania wote wenye sifa tajwa hapa chini nafasi za ajira katika Halmashauri ya Wilaya ya LIndi

Afisa Mtendaji Wa Kijiji Daraja III-Nafasi 11
Sifa za Mwombaji
(i) Awe na elimu kidato cha IV/V
(ii) Awe amehitimu Astashahada katika fani ya utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali
(iii) Awe na umri wa miaka kuanzia miaka 18 na isizidi miaka 45
(iv) Awe ni Mtanzania
(v) Awe amepata mafunzo ya kompyuta

Kazi na Majukumu ya kufanya
(a) Afisa Mahusuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
(b) Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala bora katika kijiji
(c) Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
(d) Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
(e) Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lako na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali
(f) Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu katika Kijiji
(g) Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
(h) Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji
(i) Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
(j) Kusimamia utungaji wa Sheria NDogo za Kijiji na
(k) Atawajibika kwa Mtendaji Kata

Ngazi ya Mshahara
Cheo hiki kinaanza na ngazi ya Mshahara wa TGS B kwa mwezi

NB: MAELEZO YA JUMLA

i. Waombaji wenye sifa, taaluma na uwezo waandike barua zao kwa mkono waambatanishe nakala za vyeti vyao vya kuhitimu shule na mafunzo (vyeti) vinavyoonyesha kiwango cha kufaulu na siyo "leaving certificate", pamoja na nakala ya cheti cha kuzaliwa
ii. Maelezo binafsi (CV) na nyaraka zote muhimu pamoja na picha (passport size 2 ) zilizopigwa karibuni
iii. Ili kurahisisha mawasiliano kwa nafasi hizo waombaji wote wanasisitizwa kuonyesha namba zao za simu ya mezani, mkononi au "Fax Na" chini ya anwani yake
iv. Waombaji ambao wapo katika ajira wanasisitizwa kupitisa barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa
v. Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri kati ya miaka 18-45

Jinsi ya kutuma maombi


APPLICATION INSTRUCTIONS:

i. Maombi yote yaandikwa kwa mkono
ii. Pia mwombaji aambatanishe CV yake
iii. Anuani anayopatikana kiurahisi, namba ya simu ya mkononi, Barua pepe
iv. Nakala ya vyeti vya Elimu ya Sekondari, Vyeti vya vyuo na cheti ya Kompyuta
v. Picha 2 ndogo (passport size) za rangi za hivi karibuni

Kwa yeyote mwenye sifa kama iliyoainishwa hapo juu atume maombi kwa njia ya posta kwa anwani iliyopo hapa chini na mwisho wa kupokea maopmbi ni tarehe 16/03/2015 saa 9:30 Mchana. Barua zitakazoletwa ofisini kwa mkono hazitapokelewa

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya LIndi
S.L.P 328
LINDI

NB:
- Hati ya Kiapo/hati ya matokeo wala taarifa ya matokeo havitakubaliwa
- Waombaji walioajiriwa wapitishe barua zao za maombi kwa waajiri wao

Tangazo hili limetolewa na

Vavunge, O
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya wilaya ya Lindi


0 comments:

Post a Comment