Tuesday, December 30, 2014

KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (NAFASI 5)



KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (NAFASI 5)
HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji (W) Ulanga anawatangazia wananchi wote walio na sifa kwamba  nafasi za kazi kama zifuatavyo
NAFASI; KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (NAFASI 5)
SIFA
•    Awe amehitimu kidato cha Nne au Sita na kutunukiwa cheti
•    Awe amehitimu na kufaulu mafunzo ya Uhazili au Chuo chochote kinachotambuliwa na serikali na kufuzu Mtihani wa hatua ya tatu
KAZI ZA KUFANYA
•    Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
•    Kusaidia kupokea wageni na kuwaelekeza
•    Kutunza taarifa mbalimbali
•    Kusaidia kutafuta majalada na nyaraka mbalimbali
MSHAHARA; kiwango cha mshahara ni ngazi ya TGS.B yaani 345,000/= kwa mwezi
MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI
•    Awe ni raia wa Tanzania
•    Awe na umri wa miaka 18-41
•    Awe hajawahi kuhukumiwa na kufungwa/kukabiliwa na kosa la jinai au kufukuzwa kazi.
•    Watumishi wa umma walioajiliwa hawapaswi kuomba
•    Maombi yote yaandikwe kwa mkono na kuambatanisha makala za vyeti vya Shule na taaluma, passport size mbili (2)
•    CV
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15/01/2015 saa 9:30 Alasiri na maombi yote yatumwe kwa anwani
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
S.L.P 22
MAHENGE/ULANGA


0 comments:

Post a Comment