Saturday, September 27, 2014

FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN GEOMETRIC) – NAFASI 25-ZINARUDIWA



FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN GEOMETRIC) – NAFASI 25-ZINARUDIWA


Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/0325 Septemba, 2014

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 102 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Maji,
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Oktoba, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika
Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,
Secretariat,
SLP.63100,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aoyesajiliwa ili
aweze;
 Kushirikiana na Wahandisi wa Maji na kuwaongoza walengwa katika kuchagua njia za
kupitisha bomba kwa ajili ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
 Kupima hali ya kijiografia ya maeneo ya inayokusudiwa kujengwa au yenye miradi ya
maji na usafi wa mazingira ili kuwezesha usanifu wa miundo mbinu miradi;
 Kupima uwekaji wa vifaa vya miundo mbinu kwenye ardhi wakati wa ujenzi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira;
 Kunakili na kutunza taarifa za upimaji wa ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya miradi ya
maji na usafi wa mazingira kwa namna inayokubalika kwa mchoraji wa ramani za usanifu
wa miradi kufanya kazi yake kwa unadhifu;kuchora ramani za maeneo ya miradi ya maji
na usafi wa mazingira kwa namna zote zinazokubalika kwa ajili ya kuwezesha usanifu
wa miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira;
 Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za upimaji ardhi.
SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Water Works Technician Geometric).
MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.


.













0 comments:

Post a Comment