Monday, August 26, 2013

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AWATAKA WAFANYA KAZI KATIKA MAHOTELI KUSAIDIA KUWAFICHUA WAHALIFU



MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AWATAKA WAFANYA KAZI KATIKA MAHOTELI KUSAIDIA KUWAFICHUA WAHALIFU
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Said Meck Sadik amewataka wafanyakazi katika mahoteli kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama iwapo wataona kuna mteja wao wanayemhisi kuwa ni muhalifu kwa kutoa taarifa kunakohusika mara moja.
Mhe Sadiki alitoa rai hiyo wakati wa uzinduzi wa Hoteli ya kisasa ya Nemax Royal Hotel iliyopo wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam.
Amesema katika nchi nyingine wafanyakazi wa mahoteli wamekuwa mstari wa mbele katika kulinda nchi zao kwa kutoatoa taarifa kwa vyombo vya usalama iwapo wanaona mteja aliyepanga katika hoteli yao si mtu salama
Amesema kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha usalama wa nchi Mkuu huyo Bwana
 Mkuu wa Mkoa Said Meck Sadiki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Hotli ya Nemax Royal Hotel kulia kwake ni Mkurugenzi mkuu wa hoteli hiyo bwana Rupia Jonathani Rupia
Hoteli ya kisasa ya Nemax Royal Hotel iliyopo wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Said Meck Sadik akihutubia katika sherehe hizo
Mkuu wa Mkoa katikati akishirikina na Mkurugenzi mkuu wa Nemax Royal Hetel Rupia Jonathani Rupia pamoja na mkewe mama  Jonathan Rupia katika kukata keki ya uzinduzi wa hoteli hiyo picha na Chris mfinanga



0 comments:

Post a Comment